2 Aprili 2012 - 19:30

ABNA inatutaafifu kuwa:Wananchi wa Senegal wameopata rais mpya, ambaye ameapishwa wiki moja baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa.

Macky Sall 50, aliapishwa kuwa rais wa Senegal baada ya kumshinda aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abdullaye Wade katika uchaguzi uliofanyika mara ya pili baada ya uchaguzi wa kwanza kutotoa mshindi  na hatimaye kumtoa kwenye kiti rais huyo aloongoza kwa muda mrefu.Macky Sall alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura asilimia 66% na Wade alipata asilimia 34%.